mhe.salim hemed alipoanguka na kubebwa na wabunge wenzake.
WASIFU WA MAREHEMU SALIMU HEMED KHAMIS – ALIYEKUWA MBUNGE WA CHAMBANI - PEMBA KWA TIKETI YA CUF, ALIYEFARIKI 28/03/2013. KUZALIWA; Mhe. Salimu Hemed Khamis(Marehemu) alizaliwa shehia ya Mizingani jimbo la Chambani tarehe 20 Septemba 1951 . ELIMU YA MSINGI; • Mwaka 1959-1960 alisoma katika shule ya msingi Pandani. • Mwaka 1960 – 1967 alisoma katika shule ya msingi Kengeja na kuhitimu elimu ya msingi. ELIMU YA SEKONDARI;
• Marehemu alijiunga na masomo ya sekondari mwaka 1968 katika shule ya
Sekondari ya Chambani iliyoko Pemba na alisoma hapo hadi mwaka 1969.
• Ilipotimu mwaka 1970 marehemu aliendelea na masomo ya sekondari
katika shule ya sekondari ya Fidel Castro na alihitimu mwaka 1971.
• Mwaka 1972 marehemu alijiunga Lumumba Sekondari, zamani ikiitwa
“LUMUMBA COLLEGE” kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano sita na
alihitimu mwaka 1973. ELIMU YA JUU; • Marehemu alisomea shahada ya kwanza Bachelor of Science in Agronomy 1978 -1982 huko Havanna nchini Cuba.
• Mwaka 1988 – 1989 alijiunga na chuo cha Commonwealth Mycological
Institute kilichoko nchini Uingereza (UK) na kusomea shahada ya uzamili
ya masuala ya “Plant Disease Management” yaani “utaalamu wa magonjwa ya
mimea” MAFUNZO YA KITAALAMU; • Mwaka 1987 - Marehemu
alishiriki na kuhitimu mafunzo ya uongozi ya “SENIOR MANAGEMENT COURSE
ON AGRICULTURE” huko nchini Uswisi. • Mwaka 1989 - Marehemu
alishiriki mafunzo maalum ya “UTAFITI WA VIRUTUBISHI WA MIMEA” yaani
“IDENTIFICATION OF PATHOGENIC FUNGI AND BACTERIA” katika chuo cha
“Commonwealth Mycological Institute” CMI huko LONDON - Uingereza, UTUMISHI WA UMMA;
Marehemu ametoa mchango mkubwa katika sekta ya umma kwa upande wa
Zanzibar na Tanzania Bara kutoka na elimu kubwa na adimu aliyojaliwa na
mwenyezi mungu sambamba na ujuzi; • Marehemu alikuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Mtambile Pemba chini ya wizara ya elimu mwaka 1974 – 1978. • Mwaka 1977 – 1978 alifundisha pia katika Shule ya Sekondari Fidel Castro – Pemba.
Katika kusukuma gurudumu la kilimo ambalo ndilo uti wa mgongo wa taifa,
marehemu alitumia ipasavyo utaalam na ujuzi wake wa hali ya juu wa
masuala ya usimamizi wa mimea kwa kusimamia mashamba kadhaa ya kilimo; • Mwaka 1984 - 1996 alikuwa meneja wa shamba la Shirika la Sukari na Manukato la Mahonda lililoko Zanzibar.
• Mwaka 1997 hadi 2001 marehemu alikuwa meneja wa shamba la Kampuni ya
SAS rasmi likijulikana kama SAS Company Ltd lililokuwa mkoani Morogoro. KUJIUNGA NA SIASA NA KUWA MBUNGE.
• Marehemu alijiunga na The Civic United Front - CUF Chama Cha Wananchi
kama mwanachama hai mwaka 1997 na alikitumikia chama kwa uaminifu na
jitihada kubwa. • Mwaka 2005 marehemu Salim Hemed Khamis
alipitishwa na Chama Cha Wananchi CUF kuwa mgombea ubunge katika jimbo
la Chambani na alishinda uchaguzi wa Oktoba 2005 na kuwa mbunge halali
wa jimbo hilo. • Mwaka 2010 alipitishwa tena chama ili akiwakilishe
katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilohilo na alishinda
tena na kuongoza kipindi cha pili hadi umauti ulipomkuta. • Alikuwa
Waziri Kivuli wa Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika tangu Mwaka 2005
hadi 2010 Bunge la Tisa lilipo maliza muda wake NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA;
Kutokana na uwezo wake mkubwa katika masuala ya uongozi, chama
kilimpatia marehemu Salim Hemed Khamis dhamana kubwa za uongozi; • Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa tawi la Kimbuni tangu mwaka 1997 hadi anafariki.
• Mjumbe wa Kamati ya Utendaji jimbo la chambani na Mjumbe Kamati ya
Utendaji ya Wilaya ya mkoani Pemba tangu mwaka 2005 hadi anafariki. • Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CUF taifa mwaka 2011 – 2012.
• Marehemu alikuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa 2005 hadi anafariki
na mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa - CUF tangu mwaka 2011 hadi
2012. • Marehemu alikuwa Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi kwa
ngazi ya taifa mwaka 2011 na kwa namna ambavyo alithamini masuala ya
uongozi, ilipofika mwaka 2012 aliomba kupumzika wadhifa wa Ukurugenzi
wa kitaifa ili aelekeza nguvu zaidi jimboni jambo ambalo liliridhiwa na
chama. Hadi anafariki marehemu ameacha vizuka wawili na watoto wanane.
"CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMEPOTEZA NGUZO MUHIMU, TUNAWASHUKURU
WATANZANIA WOTE WANAONDELEA KUTUMA SALAMU ZA POLE KWA VIONGOZI WA CHAMA
NA WAFIWA".
| | | | | | | | | | |
|
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment